Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeazimia kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF Development Trust Fund).
Uamuzi
wa kuanzisha mfuko huo umepitishwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF
iliyokutana Mei 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo madhumuni yake ni
kutafuta vyanzo vya rasilimali za kuendeleza programu za mpira wa miguu Tanzania.
Mfuko
huo utakaokuwa chini ya uenyekiti wa Rais aliyepita wa TFF, Leodegar Tenga
utatafuta rasilimali za kuendeshea michuano ya Taifa na kimataifa ya wavulana
na wasichana kwa vijana wenye umri chini ya miaka 13, 15, 17 na 19.
Pia
kuendeleza maeneo ya ardhi kote Tanzania ambayo ni mali ya TFF kwa kujenga
vituo vya michezo (sports centres), kutafuta rasilimali za kutoa mafunzo kwa
makocha, marefa, madaktari wa tiba ya michezo na viongozi (administrators).
Majukumu
mengine ya mfuko huo ni kuagiza na kusambaza vifaa vya michezo hasa kwa watoto
wadogo (grassroots) na vijana.
Mfuko
huo utazinduliwa Oktoba 8 mwaka huu ambayo ni siku ya kilele cha Tanzania
kutimiza miaka 50 ya uanachama wake katika Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA).
Mbali
ya Tenga, wajumbe wengine wanaounda bodi ya mfuko huo ni Mwenyekiti wa zamani
wa Simba, Ayoub Chamshama, Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Fredrick Mwakalebela,
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Tarimba Abbas na Mbunge wa
Viti Maalum, Zarina Madabida.
0 COMMENTS:
Post a Comment