May 17, 2014



 UKIANGALI hata kwenye mtandao wa Ligi Kuu England maarufu kama Premiership, eti hata wao hawajui Gnegneri amezaliwa katika mji gani, kichekesho!

Amezaliwa kwenye mji wa Bouake nchini Ivory Coast, wala si kitu cha kutafuta, lakini inaonekana ni kiasi gani wasivyotaka kufuatilia na hiyo ni moja ya sifa moja kuonyesha wao ni wabaguzi.
Yaya amelalamika mara tu baada ya kwisha kwa Premiership, kwamba alistahili tuzo angalau moja, lakini katoka kapa.
Mchezaji mwenzake Samir Nasri amelisema hilo, ana haki ya kusema hivyo. Lakini Waingereza wanatamani alichokifanya msimu huu ingekuwa Rooney, wamebugi.
Jamaa alikuwa fiti katika kuchezesha, ulinzi na hata mabao amefunga 20 akizidiwa na washambuliaji wawili tu wa Liverpool Luis Suarez (mabao 31) na Daniel Sturridge (mabao 21). Lakini wengine wote zaidi ya 30 kutoka katika timu 20 wakiwemo wa Man City anawazidi.
Katika mabao 20 aliyofunga kwa msimu huu, Yaya hajafunga hata moja katika kipindi cha kwanza, hii inaonyesha kila muda unavyokwenda, akili yake inazidi kuongeza ubunifu.
Lakini hiyo haitoshi, pamoja na kuongezeka ubunifu wakati wengine wanachoka, inaonekana mapafu yake huongeza uwezo wa kufanya kazi kila wengine wanavyozidi kupungua kutokana na uchovu.
Kwani pamoja na mabao 20 aliyofunga yote yakiwa katika kipindi cha pili, Yaya amefunga mabao 14 katika dakika ya 90.
Hii inaonyesha wakati kila mmoja anakata tamaa kuwa muda umekwisha, Yaya ndiyo anaamka na kazi yake inaisha hadi filimbi ya mwamuzi.
Lakini bado ni mfano wa kuigwa kwamba, ana kilo 90 lakini mwili wake ameuandaa vema, kiwango ni cha juu, hivyo ukizubaa anafunga.
Moja ya mabao bora kabisa aliyofunga ni dhidi ya Aston Villa, pia lilikuwa ni katika dakika ya 90 na aliwatoka mabeki watatu tokea nyuma ya katikati ya uwanja na kwenda kufunga.
Sasa vipi asipate tuzo, kwa kuwa mweusi, au kwa kuwa anatokea Afrika? Huo ni ubaguzi.

Umri: Miaka 31
Urefu: Sentimeta 189
Weight: Kilo 90
Msimu wa 2013-14
Mechi Mabao  asisti   mashuti
35           20            9           64
Shambulia
    79
Ulinzi
  79
Kiwango cha Juu
     9.45
Kiwango cha chini
    5.99
Wastani
 7.2
Premiership
Mechi 134
Mabao 41
Kadi njano 21
Kadi nyekundu 0
Makombe 2
Misimu 3


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic