May 5, 2014




SIFA ya mchezo wa soka ni kuwa na fitna katika kila upande, ingawa hapa nyumbani wengi wamekuwa wakipambana katika kugawana mapato au wizi wa mapato milangoni.

Fitna kubwa ipo kwenye fedha, hilo halina ubishi, ndiyo maana limeanzisha hadi makundi kama yale ya wanachama waliojipachika ukomandoo wa bila mafunzo, lakini yote ni fitna.

Baadhi ya viongozi wamekuwa wakiwatumia kufanya fitna ya mambo mbalimbali na kujiingizia kipato pia lakini kama unataka kujua fitna za kisayansi, basi ni zile zinazoendeshwa na wakala maarufu wa wachezaji, Pinah Zahavi.
Huyu ni maarufu kama Pini, ni wakala wa kuuza wachezaji anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), ingawa jamaa huyu kitaaluma ni mwandishi wa habari za michezo.
Pini, raia wa Israel, sasa ni maarufu na amekuwa akitumiwa kila sehemu inayoonekana kuna ugumu na makocha maarufu kama Alex Ferguson, Ron Atkinson, Terry Venables wamekuwa wakimtumia kuhakikisha wanawapata wachezaji kila kunapokuwa na fitna.

Kawaida wakala huyo amekuwa akiingia kuvuruga uhamisho katika hatua za mwisho kabisa, ndiyo maana utasikia kuwa mchezaji fulani anajiunga a Manchester United, halafu ghafla unasikia ametua Chelsea tena katika hatua za mwisho.
Inaelezwa Pini hadi sasa ametengeneza kitita cha jumla ya pauni milioni 111 (zaidi ya shilingi bilioni 240) kupitia kushiriki katika uhamisho wa wachezaji mbalimbali duniani ambao ulikuwa na mafanikio.
Lakini amekuwa akilaumiwa kutokana na tabia yake ya kuficha kipato anachopata katika sehemu ya uhamisho mbalimbali ukiwemo ule wa mshambuliaji Didier Drogba ambaye alitokea Marseille na kujiunga na Chelsea.
Pini sasa ni kati ya wanamichezo mamilionea na alishaachana na uandishi wa habari na kujikita zaidi katika kazi hiyo na inaelezwa ndiye wakala anayeaminika zaidi kutokana na kuwa na urafiki na makocha wengi maarufu, lakini urafiki na wamiliki wa timu na mamilionea kama Roman Abramovich wa Chelsea.
Alianza kuchanganya na kazi hiyo taratibu akiwa mwandishi katika Gazeti la Hadashot Hasport kwa kuwahamisha wachezaji waliokuwa wanacheza Ligi Kuu Israel kwenda England na kwingineko duniani na akawa analipwa ada ya kuwakutanisha makocha na makocha au timu na timu.
Mambo yalipochanganya, Pini ambaye baba yake alikuwa ni muuza duka, mwishoni mwa miaka 1980, akaamua kuachana na uandishi na kujikita kwenye uwakala na haraka kutokana na ujanja na kuwa mjuzi wa fitna akajulikana haraka na kujenga jina lake na sasa ndiye gumzo kwa mawakala.
Kuna uhamisho mbalimbali ambao ameshiriki baada ya kuamua kuachana na uandishi wa habari lakini kuna baadhi ilikuwa gumzo kama hii ifuatayo.

Rio Ferdinand:
Rio ni kati ya wachezaji wake na amepata mamilioni ya pauni kwake, kwani alimhamisha kutoka West Ham kwenda Leeds mwaka 2002 kwa pauni milioni 18, halafu akamtoa Leeds kwenda Man United kwa pauni milioni 30 na yeye akapata zake pauni milioni 1.13 (zaidi ya Sh bilioni 2.5).

Jaap Stam:
Kutokana na urafiki wake na Ferguson tangu mwishoni mwa miaka ya 1980 alipotua Man United, Pini alikuwa anaaminiwa sana na kocha huyo.
Alishiriki zoezi lote la kumuuza Jaap Stam kutoka Man United na kwenda Lazio kwa pauni milioni 16.5 na baadaye Ferguson alisema kwamba alijuta kumuuza beki huyo Mholanzi ambaye alikuwa jembe.

Juan Veron:
Mwaka 2001, Pini alikuwa mtamboni tena katika biashara ya kumuuza Juan Sebastian Veron kutoka Lazio na kujiunga na Man United kwa dau kubwa la pauni milioni 28.1.

Eriksson:
Pini akaendelea na kazi yake pale alipomshawishi kocha kijana enzi hizo, Sven-Goran Eriksson kutoka Benfica na kujiunga na Lazio.
Mzozo ulikuwa mkubwa kwa kuwa baadaye alitoka Lazio kwenda Sampdoria kwa kuwa timu hizo zina upinzani mkubwa. Yeye alijuana na Eriksson wakati akiwa kocha kijana katika kikosi cha timu ya Benfica.

Ashley Cole:
Zoezi la Ashley Cole kutoka Arsenal kwenda Chelsea lilikuwa na utata mkubwa baada ya mchezaji huyo kukutana na Jose Mourinho na bosi wa Chelsea, Peter Kenyon. Cole alikuwa na wakala wake, Jonathan Barnett.
Barnett alifungiwa miezi 18 kwa kosa la kushiriki zoezi hilo haramu, lakini ikaelezwa Pini ndiye alichonga mipango yote, halafu mwisho akawa msafi na adhabu haikumgusa hata kidogo na mwisho Cole akatua Chelsea. Ameshiriki karibu kila uhamisho uliohusisha fitna za juu.
UHAMISHO ALIOCHAKACHUA:
*Alama ….inawakilisha fedha ya Pauni ya England.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic