Kocha wa timu ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka
20 ya Tanzania, Ngorongoro Heroes amesema walizidiwa na wapinzani wao Nigeria
hadi kuchapwa mabao 4-1.
Kwa kipigo hicho maana yake Watanzania wameng’oka kwa jumla ya
mabao 6-1 katika michuano hiyo kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika.
Katika mechi ya kwanza, Ngorongoro ilikubali kulala nyumbani kwa
mabao 2-0.
Hata katika mechi ya jijini Dar, Wanaigeria walionyesha
kujipanga zaidi na kuwapa wakati mgumu Ngorongoro.
0 COMMENTS:
Post a Comment