May 27, 2014


DOKTA NDUMBARO (KATIKATI) AKIZUNGUMZA KUHUSIANA NA KUENGULIWA KWA WAMBURA. WANAOMFUATILIA KWA MAKINI NI WAJUMBE WA KAMATI YA UCHAGUZI YA SIMBA.

Uamuzi wa Kamati ya uchaguzi ya Simba kumuengua mgombea wa urais, Michael Wambura, umetokana na mgombea huyo kumamatwa na mapingamizi mawili.

Wambura aliwekewa mapingamizi sana na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba, Dokta Damas Daniel Ndumbaro amesema, mapingamizi matano waliyatupa na mawili yakamkamata.
Akizungumza leo mchana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dokta Ndumbaro ambaye ni mwanasheria maarufu nchini, alisema Wambura aliwekewa mapingamizi saba.
"Mapingamizi matano tumeyatupa, mawili ndiyo yamemuengua Wambura katika uchaguzi huo wa Simba," alisema.
Uchaguzi wa Simba umepangwa kufanyika Juni 29 na sasa wagombea wa Urais wamebaki Evans Aveva na Andrew Tupa.
Hata hivyo, Wambura ana nafasi ya kukata rufaa kwenye kamati ya rufaa ya TFF ambayo imeelezwa inaweza kumsaidia kutokana na kuwa na rafiki zake wengi.
Mapingamizi 'yaliyomkamata' ni lile la kuipeleka Simba mahakamani miaka michache iliyopita, la pili ni lile la kuvuliwa uanachama wake.
Hivyo, Wambura alitakiwa kurudishwa uanachama na mkutano wa Simba ambao haukuwahi kukaa hata siku moja kufanya jambo hilo.
Wambura aliwahi kuwa mwenyekiti wa muda wa Simba mwaka 2011, lakini kabla ya hapo, mwanzoni mwa miaka ya 2000 alikuwa Katibu Mkuu wa TFF baada ya kumshinda Ismail Aden Rage.
Hata hivyo, mambo yalimuendea vibaya baada ya kusahau kutuma majina ya timu mbili za Tanzania zilizotakiwa kushiriki michuano ya kimataifa, aliposhituka, muda wa kutuma ulikuwa umepita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic