Kocha Mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger
amesisitiza anataka kubaki katika kikosi hicho alichoanza kukinoa mwaka 1996.
Wenger aliingoza Arsenal kwa muda wa siku
3,283 bila ya kubeba kombe, hali iliyosababisha mzozo mkubwa na masimango
kwake.
Lakini mwisho, amekata mzizi wa fitna kwa
bao la Ramsey ambalo lilikuwa la tatu na kuiwezesha Arsenal kushinda kwa 3-2
dhidi ya Hull City na kubeba Kombe la FA.
Wenger amesema: “Siku zote nimekuwa
nikisisitiza, kombe haliwezi kuwa kipimo kwangu kama naondoka au nabaki.
“Lakini nimekuwa nasisitiza kuwa nataka
kubaki Arsenal, hili si jambo geni hata kidogo.
“Kikubwa leo ni kuwapongeza wachezaji
walivyopambana kutoka chini kwa mabao mawili hadi kuibuka na ushindi.
“Kikubwa kwetu kilikuwa ni ubingwa, ilikuwa
ni lazima kushinda na tumefanya hivyo,” alisema Wenger.
Mara ya mwisho Arsenal ilitwaa Kombe la FA
mwaka 2005 na ndilo kombe lao la mwisho kabla ya jana usiku kuishinda Hull na
kubeba hilo ambalo linakuwa la tano kwa makombe ya FA aliyobeba.
0 COMMENTS:
Post a Comment