Mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar, leo, Stars ilipata bao lake mapema katika kipindi cha kwanza
kupitia John Bocco.
Baada ya hapo, Zimbabwe walibadilika na
kuwa moto kwa Stars kwa kipindi chote cha kwanza.
Stars walikosa mara kadhaa nafasi
kupitia kwa Bocco, Mbwana Samatta.
Mshambuliaji wa TP Mazembe, Thomas
Ulimwengu ndiye alionekana kuwa tishio zaidi kwa Wazimbabwe hao.
Hata hivyo, kipindi cha pili haikikuwa
kizuri kwa Taifa Stars kwani kipa Deo Munish ‘Dida’ alilazimika kufanya kzi ya
ziada mara kadhaa.
Mabeki Kelvin Yondani, Nadir Haroub,
Shomari Kapombe na Oscar Joshua na walipambana vilivyo kuiokoa Stars.
0 COMMENTS:
Post a Comment