LOGA AKIWA NA MCHUNGAJI MOSHA |
Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic ametoa zawadi ya jezi ya Simba kwa mchungaji wa
kanisa la Katoliki ambaye ni mshabiki wa Yanga na akaipokea bila ya matatizo.
Logarusic
maarufu kama Loga amewasilisha zawadi hiyo siku tatu katika mji aliozaliwa wa
Slavonski Brod ambao mchungaji, Josephat Mosha amekuwa akifanya kazi kwa miaka
nane sasa.
Mosha
raia wa Tanzania ambaye anatokea mkoani Arusha amekuwa akifanya kazi nchini
humo kwa miaka nane na alikutana na Loga baada ya kusikia amekuwa akifanya kazi
nchini.
“Kweli,
mchungaji ni mtu mwema sana, alinitafuta kwa juhudi akitaka tukutane, mwisho
ikawa hivyo na tulikula chakula cha usiku pamoja kwa mwaliko wake,” alisema
Loga.
“Baada
ya hapo sikuwa na zawadi ya kumpa zaidi ya jezi ya Simba, ingawa aliniambia ni
shabiki wa Yanga, lakini aliipokea kuonyesha utaifa. Watanzania ni watu
waungwana sana na mchungaji Josephat ni sehemu ya mfano.”
Mchungaji
Mosha ameishi nchini humo kwa miaka nane, hata hivyo sasa amehamia katika eneo
tofauti na mji wa Slavonski Brod aliozaliwa Loga.
Sasa
anaishi na kufanya kazi katika mji wa Sibenik ambao uko kilomita 400 kutoka
Slavonski Brod ambako ameishi kwa miaka saba.
Loga
yuko kwao Croatia kwa ajili ya mapumziko na amekuwa akisubiri uchaguzi mkuu wa
Simba ili arejee kazini.
Kocha
huyo aliichukua Simba chini ya Abdallah Kibadeni, lakini ikamaliza ligi ikiwa
nafasi ya nne na ameahidi iwapo ataanza nayo msimu, basi ana uhakika itakuwa
bingwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment