Kamati ya rufaa ya TFF
itakayosikiliza rufaa ya mgombea wa urais Simba, Michael Wambura aliyeenguliwa
kwenye uchaguzi, imewaalika wajumbe wa kamati ya uchaguzi ya Simba.
Wajumbe wa kamati ya uchaguzi na
Mwenyekiti wao Damas Daniel Ndumbaro ‘DDN’, wameombwa kufika kwenye kikao hicho
cha kesho mchana.
Kesho ndiyo siku ambayo kamati hiyo itakuwa inapitia rufaa ya Wambura anayepinga kuondolewa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi baada ya kuondolewa kwa mara ya pili baada ya kubainika alifanya kampeni kabla ya muda wake.
Awali kamati hiyo ilikata rufaa
iliyokuwa isikilizwe na kamati ya maadili ya TFF, lakini Rais wa shirikisho
hilo, Jamal Malinzi akaibuka na kutaka iundwe kamati ya maadili ya Simba, kitu
ambacho kimeonekana ni kuvuruga uchaguzi na tayari wanachama wa Simba
wamelipinga hilo.
Safari hii, kamati ya rufaa ya TFF
imekubali kuwaita wajumbe wote wa kamati ya uchaguzi ambao wamemuengua Wambura
kwa mara ya pili baada ya kubainika alifanya kampeni kabla ya muda wake.
Kabla ya hapo kamati hiyo
ilimuonyesha Wambura na mgombea mwenzake, Evans Aveva kutoshiriki matendo ya
kampeni kabla ya kipindi sahihi, lakini Wambura akafanya hivyo baada ya
kuenguliwa mara ya kwanza na pale aliporudishwa na kamati ya rufaa.
Wambura amekata rufaa juzi na
kamati hiyo inakutana kuisikiliza rufaa yake kesho, ndani ya siku tatu kila
kitu kimekwenda kama kilivyopangwa.
Kamati hiyo ya rufaa ya TFF,
itasikiliza rufaa hiyo kesho na taarifa zinaeleza uamuzi utatolewa keshokutwa
Ijumaa.
0 COMMENTS:
Post a Comment