Mwanachama na mfadhili wa
zamani wa Simba, Azim Dewji amesema ana uhakika kamati ya rufaa ya Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), itamrudisha kugombea, Michael Wambura.
Wambura aliondolewa na
kamati ya uchaguzi ya Simba ambayo ilieleza sababu za msingi kuwa amebainika
uanachama wake una walakini.
Lakini Wambura, hajawahi kuzipangua kwa hoja pointi hizo zilizotolewa na kamati ya uchaguzi ya Simba, zaidi ya kuonyesha makali yake kwa maneno na baadaye kukata rufaa.
Kamati ya rufaa ya TFF inakutana kesho kujadili rufaa ya Wambura na nyinginezo na ndiyo kumekuwa na fununu kwamba atarudishwa kwa kuwa alikuwa ndiye meneja wa kampeni za Malinzi.
Akizungumza leo katikati ya jiji la Dar es Salaam, Dewji aliyekuwa mfadhili wakati Simba inafika fainali ya Kombe la Caf mwaka 1993, alisema TFF imekuwa na maamuzi ya kuimiza Simba kila mara.
Aidha, alisema Rais wa TFF,
Jamal Malinzi na Wambura ni marafiki na Wambura alifanya kazi ya ukampeni
meneja kwa Malinzi, hivyo kamati haitafanya kazi kwa uhuru zaidi ya kumridhisha
Malinzi aliyeichagua.
“Kwanza imekuwa ni kawaida
ya TFF kufanya maamuzi ambayo yanakuwa na maumivu kwa Simba, lakini ukiachana
na hivyo, si siri ndugu yangu, kila mtu anajua Wambura alikuwa meneja wa
kampeni za Malinzi kuingia TFF.
“Sasa unafikiri ile kamati
itakuwa huru kufanya uamuzi ambao ni sahihi kama ule wa kamati ya uchaguzi ya
Simba. Hoja za kamati ya uchaguzi ziko wazi, hakuna kilichofichika.
“Lakini mimi nasema leo,
kwa kuwa kamati inakutana kesho, basi mtanipa jibu. Wambura atarudi, ndiyo
maana nimejitokeza leo kuwaambia wanachama hata kama wamepanga kumrudisha kwa
hila, wanachama wawe makini, wasimchague,” alisema Dewji.
Kumekuwa na upinzani mkubwa
kati ya Evens Aveva na Wambura ambao watachukuana katika nafasi ya kuwania
urais wa Simba.
Hata hivyo, Aveva amekuwa
akipewa nafasi huku ikiamini Wambura kama kweli atarudishwa na TFF kama
alivyosema Dewji, anapewa nafasi ya pili kuweza kuchukua nafasi hiyo ya urais.
0 COMMENTS:
Post a Comment