Kiungo wa zamani wa Simba, Hamis Soda amemtaka mgombea aliyeenguliwa
kwenye kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya urais katika klabu hiyo, Michael
Wambura kukaa pembeni na kuwaachia wengine.
Wambura kwa sasa anasubiri hatma yake ya kugombea nafasi hiyo baada ya
kukata rufaa kwenye Kamati ya Uchaguzi ya TFF huku hukumu yake ikiwa ni Juni 9,
mwaka huu.
Soda amesema kuwa kutokana na Wambura kuenguliwa kwenye nafasi hiyo,
basi hana budi kukaa pembeni na kuwaachia wengine ili kulinda heshima yake.
“Wambura anachotakiwa kwa sasa ni kuachana na uongozi kwa sababu siyo
mara ya kwanza kuwekewa mapingamizi na kama ningekutana naye, ningemshauri
apumzike mpaka miaka minne ipite,” alisema Soda ambaye aliichezea Simba mwaka 1974
mpaka 1985.
0 COMMENTS:
Post a Comment