June 6, 2014



Makamu Mwenyekiti wa Tawi la Simba la Magomeni Makucha, Gadner Hatwaby Dibibi amesema tawi lake litampa kura mgombea urais wa klabu hiyo, Evans Aveva huku wakimtaka Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ anayewania nafasi ya umakamu, aendelee kuwa kocha tu na siyo kiongozi.
DIBIBI


Dibibi ni mume wa msanii maarufu wa filamu Bongo na mwanamuziki Jack Pentezel ‘Jack wa Chuz’. 

Klabu ya Simba inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu Juni 29, mwaka huu wa kuchagua viongozi wapya baada ya uongozi wa Ismail Aden Rage kumaliza muda wake.

Kiongozi huyo alisema wanachama wa tawi lake wanamsapoti Aveva kwa kuwa wanatambua ni mtendaji kazi mzuri na atawapa mafanikio Simba kwa muda mfupi tu atakaokuwa madarakani.

“Mimi na tawi langu tutamsapoti Aveva,  tulitamani sana Julio angebaki kuwa kocha kwani hiyo ndiyo kazi inayompendeza kwa sababu jamaa bado yupo fiti maeneo hayo,” alisema Dibibi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic