Kiungo wa
zamani wa Simba, Arthur Mambeta, ameishutumu kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo
iliyo chini ya mwenyekiti Dk Damas Ndumbaro kuwa, haitendi haki ipasavyo, hasa
baada ya kumuengua mgombea wa nafasi ya urais, Michael Wambura.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Mambeta alisema hana imani tena na kamati hiyo kutokana
na maamuzi waliyoyafanya ambayo hayaendani na maelekezo ya katiba.
“Tulikuwa
tukiitegemea sana hii kamati kwenye masuala haya lakini sasa wameondoa imani
yao kwetu kwa haya maamuzi ya kumuondoa Wambura.
“Yaani hata
mtu ukimwambia amsikilize Ndumbaro kisha umpe katiba aisome, ataona kabisa
kwamba wanaenda kinyume na miongozo ya katiba na wanafanya maamuzi
wanayoyataka,” alisema Mambeta.
Hata hivyo, tayari Wambura ameshakata rufaa kwenye Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) kwa ajili ya kupinga kuenguliwa huko na rufaa hiyo inatarajia
kusikilizwa Juni 9, mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment