Mwenyekiti wa Tawi la Mpira Pesa, Ustaadhi Masoud,
amefunguka kuwa, mgombea wa nafasi ya urais, Michael Wambura, anatakiwa
kujiuliza na kujifunza kuwa kwa nini ni yeye tu kila wakati anakwama
anapogombea nafasi mbalimbali.
Mgombea huyo amekuwa na historia ya kukwama kila
anapojaribu kugombea nyadhifa tofauti ndani ya klabu na hata kwenye Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF).
Akizungumza jijini Dar, Masoud alisema Wambura
anatakiwa kujifunza kitu kutoka kwa wenzake kwa nini kila siku yeye anakutana
na vikwazo na si wengine.
“Nafikiri anatakiwa kujiuliza hivyo lakini sina la
kusema kwa sasa, tusubiri tu hiyo rufaa yake,” alisema Masoud.
Wambura anapambana kurejea kwenye uchaguzi huo baada
ya kamati ya uchaguzi ya Simba kumng’oa baada ya kubainika uanachama wake una
walakini.
0 COMMENTS:
Post a Comment