Juhudi za kutaka kuzuia uchaguzi kwa
kundi la wanachama wachache zimekwama na sasa uchaguzi huo mkuu wa Simba
utafanyika Jumapili kama ulivyopangwa.
Uamuzi huo umetolewa leo na Jaji
Augustine Mwarija ambaye alisema mahakama inakubali wanachama kufungua kesi
lakini inakataa kuzuia uchaguzi wa Simba kwa sababu hakukuwa na kesi ya msingi
ya madai.
Jaji Mwarija alisisitiza hivyo ombi la
zuio lililetwa kabla ya muda.
Lakini ajabu, wakili Mwenyekiti wa Rais
wa Simba, Aden Rage na wenzake wa bodi ya wadhamini, Juma Nassoro alionyesha
kusikitishwa na uchaguzi kutosimamishwa.
“Uongozi wa Simba ndiyo ulikuwa na mamlaka ya kutaka uchaguzi
uendelee au la,” alisema Nassoro na kuwashangaza wengi.
Baadhi ya wanachama waliokuwa katika
eneo hilo walionyesha kushangazwa na kusema inawezekana mwenyekiti huyo
anayemaliza muda wake alikuwa anapigia chepuo uchaguzi usimamishwe.
“Sasa Rage angefaidika na nini kama
alitaka uchaguzi usimamishwe, nimeshangazwa na maneno ya wakili wake.
“Hiki si kitu kizuri, lazima watu
waangalie maslahi ya Simba na si vinginevyo,” alisema Juma Mshamu ambaye
alisema ni mwanachama kutoka Morogoro.
0 COMMENTS:
Post a Comment