Jumla ya mikoa 30 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambao ni wanachama
wa klabu ya Simba wamepanga kuungana kwa pamoja kwa ajili ya kupinga maamuzi ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ya kusimamishwa kwa uchaguzi wa timu hiyo.
Shirikisho hilo hivi karibuni lilizuia mchakato mzima wa
uchaguzi wa timu hiyo huku likiiagiza Kamati ya Utendaji ya Simba kuunda Kamati
ya Maadili itakayopitia mapingamizi mbalimbali ya wagombea waliokatiwa rufaa.
Wanachama wa timu hiyo, walitoa kauli hiyo juzi Jumatatu
kwenye makao makuu ya timu hiyo wakimtaka Rais wa TFF, Jamal Malinzi, kuachia
mchakato mzima wa uchaguzi uendelee.
“Ujue tunashindwa kumuelewa na tunamshangaa Malinzi, sababu
iliyomfanya asimamishe mchakato wetu wa uchaguzi ni upi? Kiukweli sisi kama
wanachama hatutaki na tunamuomba atuache tuendelee na uchaguzi wetu.
“Tumeshindwa kuwa na imani naye, akumbuke kuwa sisi ndiyo
tuliowahamasisha Watanzania wote kumpa sapoti Malinzi ili aingie kuongoza soka
nchini, lakini tunashangaa maamuzi anayoyatoa kila wakati.
“Kama wanachama leo (juzi Jumatatu) tumepigiana simu za dharura
ili tukutane kwa haraka ili tupinge maamuzi ya TFF yaliyotolewa na Malinzi,”alisema
mwanachama huyo na kuongeza:
“Hivyo kama Malinzi akikataa kuurejesha uchaguzi wa Simba,
haraka tutawasiliana na wanachama wote kutoka nchini wenye kadi halali za Simba
kutoka Bara na Visiwani kwa ajili ya maandamano kupinga maamuzi hayo,” alisikika
mwanachama huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment