Mwanachama wa Simba na msanii maarufu wa Bongo Movie, Jacob
Stephen, ‘JB’, amefunguka kwamba wao kama kamati ya maombi
wanaendelea na kazi yao lakini watu wasishangae hayo yanayoendelea kwa sasa kwa
sababu ni mawimbi tu yanapita lakini kila kitu kitaeleweka hivi karibuni.
Awali mwanachama huyo alisema kuwa yeye ni mmoja na wanachama
wa klabu hiyo ambao wapo katika kamati maalum kwa ajili ya kuombea uchaguzi wa
klabu hiyo.
Msanii huyo amesema kuwa yanayoendelea kwa sasa klabuni kwao ni
kama mapito au mawimbi fulani lakini karibuni tu kila kitu kitaeleweka.
“Simba sijaona kama kuna matatizo ya kutisha zaidi sisi
tunaendelea na maombezi tu kwa ajili ya amani na utulivu kipindi hiki kwa
sababu hayo yanayojitokeza ni kama mawimbi tu.
“Wanachama wa klabu yetu wanatakiwa kuwa watulivu na
kuendelea kutafakari kwa umakini kuwa nani atakayeweza kuiongoza klabu kwa miaka
minne na ikafanikiwa na si watu kwenda kujinufaisha,”alisema JB.
0 COMMENTS:
Post a Comment