WINGA wa zamani wa timu za Yanga na
Simba, Said Maulid ‘SMG’, wiki iliyopita alimwaga wino wa kuitumikia Onze
Bravos Dos Maquis ya Angola kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya shilingi
milioni 15.
Rafiki wa karibu na mchezaji huyo amesema kwa kuwa SMG alishamalizana na uongozi kabla ya kuondoka nchini, alipofika Angola
zoezi lililobaki lilikuwa ni kumwaga wino, ambalo limekamilika wiki iliyopita
na kukabidhiwa milioni zake hizo.
Aliongeza kuwa walikubaliana mambo
kadhaa ikiwemo kuwa anaweza kuongezewa mkataba kwa ajili ya msimu ujao kutokana
na maendeleo yake klabuni hapo huku dili la kwenda kuchukua mafunzo ya ukocha
nchi za Ureno na Brazil likiwa palepale baada ya kutimiza miaka minne akiitumikia timu hiyo
iliyomaliza nafasi ya sita msimu uliopita.
“Wamempa zaidi ya milioni 15 kama ada
yake ya usajili na mkataba wa mwaka mmoja, lile dili lao lipo palepale la kwenda kwenye mafunzo
ya ukocha kati ya Brazil na Ureno lakini pia wamekubaliana kuwa wanaweza
kumuongezea mkataba kutokana na ‘performance’ yake,” alisema mtoa taarifa huyo.
SMG alitua Onze Bravos kwa mara ya
kwanza mwaka 2008 akitokea Yanga na kisha kurejea msimu uliopita kukipiga
Ashanti iliyoshuka daraja.
0 COMMENTS:
Post a Comment