DALALI (KULIA) AKIWA NA EVANS AVEVA |
Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya
Simba, Hassan Dalali, amewashukia wanachama ambao wamekuwa wakilalamikia
vitendo vya usajili vinavyofanywa kwenye klabu hiyo kwa kuwaambia wengi wao
hawajui ugumu wa kazi hiyo, lakini kama wanataka kufanya hivyo basi wasajili
wao.
Usajili wa Simba upo chini ya
mwenyekiti wao, Zacharia Hans Pope ambapo mpaka sasa tayari wameshafanikiwa
kupata saini za wachezaji Joram Nasson na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.
Akizungumza na Championi Jumamosi,
Dalali alisema wanachama hao hawajajua ni ugumu gani ambao wanaupata kwenye
usajili wa wachezaji, hivyo wanatakiwa wasipewe lawama zozote na kama watataka
kusajili wachezaji wao basi wafanye hivyo.
“Utakuta kiongozi unapewa lawama kisa
mchezaji fulani imeshindikana kusajiliwa, lakini watu hao bado hawajui ni ugumu
gani ambao tunakutana nao kwenye usajili huo, lakini kama watataka kudhibitisha
hivyo nawaambia wajaribu kusajili mchezaji mmoja ili nao waone,” alisema
Dalali.
0 COMMENTS:
Post a Comment