Kwa waliosema
wamemmiss, sasa mshambuliaji nyota wa PSG na Sweden, Zlatan Ibrahimovic ameua
nchini Brazil.
Sweden haikupata
nafasi ya kufuzu kwenye Kombe la Dunia baada ya kung’olewa na Ureno, lakini
mashabiki wengi wangetamani kumuona kwenye michuano hiyo mikubwa ya soka
duniani.
Juzi mashabiki wa
Ufaransa walibeba bango linalosema tunakukumbuka Zlatan, lakini leo amewasili
nchini humo kushuhudia michuano hiyo.
Picha za Zlatan
akiwa uwanja wa ndege na baadaye akiwa na myama aina ya Fuleco ambaye ndiye
nembo ya michuano hiy.
Haijajulikana kama
Zlatan ataangalie mpira tu kama shabiki au pia atafanya matangazo mbalimbali
akiwa nchini humo.
0 COMMENTS:
Post a Comment