June 18, 2014


 Wala usishangae, huo ndiyo mpira na sasa rasmi Hispania au Spain si mabingwa tena wa dunia.


Wamevuliwa ubingwa na wamekuwa moja ya timu zinazorudi nyumbani mapemaa.
Wamepigwa mabao 2-0 katika mechi yao ya pili ya makundi dhidi ya Chile iliyomalizika hivi punde kwenye Dimba la Maraccana jijini Rio de Janeiro, Brazil.

Maana yake wamepoteza mechi mbili za kwanza baada ya kuchapwa mabao 5-1 dhidi ya Uholanzi katika mechi ya kwanza.
Chile na Uholanzi, zimevuka kundi B, sasa zinakwenda kupambana kwenye 16 Bora.

Kwa ushindi  huo, Chile imefikisha pointi 6 sawa na Uholanzi iliyoitwanga Australia 3-2. Maana yake Hispania na Australia hata kama zitashinda mechi yao ya mwisho, zitakuwa na pointi 3, safari iko palepale.

Katika Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, mabingwa watetezi Italia nao waliishia hatua ya makundi wakiwa mkiani kabisa.
Safari hii ni kwa Hispania ambao bado wanakumbuka mabingwa watetezi wa mwaka 1998, Ufaransa ambao pia waliishia makundi mwaka 2002 Japan na Korea. Soka bana!
Adio Spain.








0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic