Nyota wa kimataifa wa Tanzania, Mwinyi
Kazimoto, anayekipiga katika Klabu ya Al Markhiya nchini Qatar, ameeleza
masikitiko
yake baada ya timu yake kushindwa kupada Ligi Kuu nchini humo.
Kazimoto, ambaye yupo nchini
kuitumikia timu ya taifa, Taifa Stars, katika mchezo wa kimataifa dhidi ya
Msumbiji, Black Mambas, utakaopigwa kesho jijini Dar. Anatarajiwa kurejea Qatar
Jumanne ijayo.
Kazimoto amesema timu yake haikupata nafasi ya kupanda ligi kuu, ambapo
iliishia nafasi ya tatu, huku sheria za nchi hiyo zikiruhusu timu mbili kupanda
daraja.
“Sikufanikiwa kucheza ligi kuu kwa
msimu mpya, ndiyo ilikuwa ndoto yangu ya kuhakikisha nami ninacheza ligi kuu,
lakini ndiyo hivyo, tulishika nafasi ya tatu, ambapo timu mbili ndizo
zinatakiwa kupanda,” alisema kiungo huyo wa zamani wa Simba.
Kwa mantiki hiyo, Kazimoto atalazimika
kusubiri msimu mwingine ili kutimiza ndoto yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment