UONGOZI wa Yanga umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Ruvu Shooting utakaochezwa Uwanja wa Mkapa kwa kuwa mwalimu Cedric Kaze amekiandaa kikosi kwa umakini.
Ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 31 inakutana na Ruvu Shooting yenye pointi 23 ikiwa nafasi ya nne na zote zimecheza jumla ya mechi 13 ndani ya Ligi Kuu Bara.
Tangu msimu wa 2010/11 zimekutana mara 18,Yanga imeshinda mara 13 na Ruvu Shooting ilishinda mara moja huku zikipatikana sare nne ndani ya uwanja kwenye mechi za ligi.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kila kitu kipo sawa ni jambo la kusubiri wakati ili kuona namna itakavyokuwa.
“Mwalimu amekiandaa kikosi chake na kipo sawasawa kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting, tunaamini kwamba utakuwa na ushindani mkubwa na wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu.
“Kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu yao kwani lengo letu ni kuona kwamba tunafikia malengo ambayo tumejiwekea ya kutwaa ubingwa,” amesema.
Mchezo wa leo utachezwa Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.
Hizo ndio mechi zenu halafu mnang'ang'ania kuangalia mechi za Simba kimataifa
ReplyDeleteUmecheza na timu ambayo haijacheza ligi miezi 7 halafu hata goli 1 hufungi nyumbani.
DeleteMueleze huyo mkia fc kuwa leo tunacheza na timu bora kuliko plateau fc na mkumbushe kuwa ruvu shooting waliwatoboa tundu moja bila majibu mpaka mwizi wa magari akarusha ngumu....dadeeeeeki
DeleteSimba inacheza kwa malengo. Lengo haikuwa goli ika kuvuka hatua inayofuata
Delete