Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete,
amepewa kibarua na kocha mkuu wa timu hiyo Mbrazili, Marcio Maximo, cha kuwa
mkalimani kwa wachezaji wenzake.
Wakati mazoezi hayo yakiendelea, kocha
huyo na msaidizi wake, Leonardo Neiva, walionekana wakimtumia mshambuliaji huyo
kuwatafsiria wachezaji wenzake kile walichokuwa wakisema.
Makocha hao wakiwa wanaendelea na
programu zao, walikuwa wakitumia Lugha ya Kiingereza na baadaye mshambuliaji
huyo kuwatafsiria wachezaji wenzake kwa Kiswahili.
Mshambuliaji huyo alilazimika
kuwatafsiria wachezaji wenzake kwa kila programu ya mazoezi iliyokuwa
inabadilishwa na makocha.
Mazoezi waliyokuwa wanayafanya ni
kukimbia mbio fupi na ndefu mchangani huku wakimalizia kwa kuruka koni.
Akizungumzia hali hiyo, Tegete alisema:
“Siyo mara ya kwanza kunipa kazi hiyo ya kuwatafsiria wachezaji wenzagu, tangu
akiwa anaifundisha Taifa Stars alikuwa ananitumia.
“Mimi nimeshazoea kwa sababu lugha
hiyo ninaijua vizuri, hivyo sioni shida kwangu, ndiyo maana muda mwingi
walikuwa wakiita na kunipa maelekezo na baadaye kuwaelezea wenzangu.”
0 COMMENTS:
Post a Comment