Baada ya uongozi mpya wa Simba kuingia
madarakani, mshambuliaji Mrundi Amissi Tambwe, amefunguka kuwa hatarejea klabuni
hapo hadi watakapokaa na kujadiliana tena kuhusiana na maslahi yake.
Tambwe ambaye msimu uliopita aliibuka
mfungaji bora baada ya kufunga mabao 19, amesema hawezi kurudi kwenye timu hiyo
hata kama ina uongozi mpya mpaka atakapotimiziwa mahitaji yake.
Simba ilifanya uchaguzi wake wikiendi
iliyopita na kufanikiwa kuwaweka madarakani Evans Aveva kama rais na Geofrey
Nyange ‘Kaburu’ kama makamu wake.
Awali, klabu hiyo ilimuahidi
mshambuliaji huyo kuwa atakaporejea msimu ujao itaboresha mkataba wake, ingawa
anasema kuwa hakuna chochote ambacho kimefanyika hadi sasa.
Akizungumza kutoka Bujurumbura, Burundi, straika huyo alisema klabu yake inahitaji kumtimizia mahitaji yake mapema kama
walivyokuwa wamekubaliana na kwa kuboreshewa mkataba, usafiri na vitu vya ndani
ndiyo aweze kuja nchini.
“Kikubwa kwa sasa nahitaji kuboreshewa maslahi yangu kuanzia
mkataba wenyewe na hata mazingira ninayoishi na usafiri pia, ili niweze kufurahia matunda ya kazi
yangu.
“Hili suala waliniahidi wenyewe, ndiyo
maana wanatakiwa kunitimizia mapema kabla hata ligi haijaanza ili kuweza
kujipanga mapema maana tunakoelekea changamoto ni wazi zitakuwa kubwa katika
ligi yetu.
Ukweli siwezi kurejea kwa sasa mpaka
nitapofahamu kuwa mambo hayo yapo vizuri,” alisema Tambwe ambaye amekuwa akiwindwa
na timu kadhaa.
0 COMMENTS:
Post a Comment