July 2, 2014



Kipa wa Yanga, Juma Kaseja, amesema hana kinyongo tena na kocha mkuu mpya wa timu hiyo, Mbrazili, Marcio Maximo na badala yake wataendelea kuitumikia Jangwani kwa roho moja.
Awali, kipa huyo akiwa kwenye timu ya taifa, Taifa Stars, aliwahi kutofautiana na kocha huyo na kusababisha kumtimua kwenye kikosi chake wakati wakiwa kambini.

Kaseja amesema kuwa tofauti zao zimemalizika hivi karibuni baada ya kukutana na kocha huyo na kuzungumza baadhi ya mambo.

Kaseja alisema atashirikiana na kocha huyo kwa kila jambo ndani na nje ya uwanja katika kufanikisha malengo yake na kuhakikisha timu yao inafanya vyema katika mashindano mbalimbali ya kimataifa na kitaifa.

“Mimi na Maximo tulikutana na kuzungumza mengi likiwemo la kumaliza ugomvi kati yangu na yeye, kikubwa aliniambia kuwa tuachane na yaliyopita na tugange yajayo katika kuipa mafanikio timu yetu.

“Tumekutana kwa mwajiriwa mmoja wote na tumekutana kwa ajili ya kufanya kazi, hivyo ninaomba tuendelee kushirikiana.

“Hivyo tofauti zangu na zake hazipo tena na tumeungana kwa pamoja, hivi sasa nguvu na akili zetu tumezihamishia katika msimu ujao kwa kuhakikisha timu inafanya vyema,” alisema Kaseja.

Maximo na Kaseja walipishana wakati wakiwa katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars na kocha huyo aliacha kabisa kumuita mchezaji huyo hadi alipoondoka kwenda kwao Brazil.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic