Mshambuliaji
nyota wa Brazil, Neymar amesema wenzake bado wana nafasi kubwa ya kumsaidia
kutimiza ndoto yake ya kutwaa Kombe la Dunia.
“Nafasi ipo, ninawaamini wenzangu wanaweza kufanya jambo na kutimiza
ndoto.
“Mimi nilikuwa ni sehemu ya timu, hivyo bado timu ina uwezo wa
kutimiza malengo yetu.
“Nawatakia wenzangu wote kila la kheri ili wafikie ndoto zetu,” alisema.
Neymar
aliumizwa na beki wa Colombia katika mechi ya robo fainali.
Beki
huyo amemvunja mfupa mdogo wa uti wa mgongo, hali inayosababisha aikose
michuano hiyo hadi mwisho.









0 COMMENTS:
Post a Comment