Kocha Hans van der Pluijm amesikitisha kutokana na kitendo
cha klabu ya Shaolla FC ya Saudi Arabia kuvunja mkataba wao kienyeji.
Pluijm raia wa Uholanzi na msaidizi wake, Charles Boniface
Mkwasa hawataendelea kuifundisha timu hiyo baada ya uongozi wa klabu kuvunja
mkataba wao.
Mkataba umevunjwa na tayari wawili hao ambao kwa pamoja
waliinoa Yanga wako katika hatua za mwisho kurejea Ghana na Tanzania.
“Ni kitu cha kusikitisha sana, kwa wiki tatu tulizofanya
kazi hapa tulikuwa tumeleta mabadiliko makubwa sana na wachezaji walikuwa na
furaha na sisi.
“Kuna wale ambao walikuwa hawana nafasi katika kikosi cha
kocha aliyepita, lakini tayari walionyesha mabadiliko makubwa.
“Tulikuwa tunategemea kuwa na kikosi kizuri baada ya
kuanza kwa ligi, lakini mambo yakaharibika baada ya viongozi mbalimbalia kuanza
kuleta wachezaji wao,” alisema Pluijm wakati akihojiwa na SALEHJEMBE.
“Tuliwafanyia majaribio wachezaji hao na kuona walikuwa na
viwango duni, tukawakataa. Hilo liliwaudhi sana viongozi.
“Baada ya siku chache wakatangaza kuvunja mkataba,
imetushangaza sana. Niseme wazi nimesikitishwa na hilo.”
Pluijm ndiye alikuwa wa kwanza kupata kazi katika klabu
hiyo, naye akampigia ‘pande’ Charles Boniface Mkwasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment