October 4, 2021


 KIPA namba moja kwa sasa ndani ya Biashara 
United, Mghana James Ssetub, amefunguka na kuuelezea mchezo wao wa kwanza na Simba ulivyokuwa mgumu na hata kusababisha wao kupata matokeo ya sare ya 0-0.


Biashara United ya Mara na Simba zilitoka suluhu hiyo kwenye Uwanja wa Karume, Musoma lakini kipa huyo amemtaja kiungo Rally Bwalya kuwa alikuwa mchezaji tishio zaidi katika kikosi cha Simba.


Akizungumza na Championi Ijumaa, kipa huyo amefunguka: “Mchezo wetu na Simba ulikuwa mzuri na mgumu sana, japo hatujapata matokeo tuliyokuwa tunayataka, tulitaka kushinda tukiwa nyumbani.


“Kwangu mchezaji bora alikuwa ni Rally Bwalya maana alikuwa anatoa mipira ya hatari sana kwa John Bocco na Meddie Kagere.

“Mipango yangu kwa Biashara msimu huu si yangu peke yangu, ni ya timu nzima na tumejipanga kuzidi kufanya vizuri ili kubaki kwenye nafasi nzuri Ligi Kuu Bara na hata kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.”

Kipa huyo aliibuka shujaa wa mchezo huo wa ufunguzi uliochezwa Uwanja wa Karume Mara kwa kuwa aliokoa hatari nne za moto zilizopigwa na Israel Mwenda pia aliokoa penalti moja iliyopigwa na nahodha wa Simba, John Bocco.

Jitihada zake zilikwama mbele ya Rashid Juma wa Ruvu Shooting ambaye alimtungua dakika ya 47 walipokutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ule wa mzunguko wa pili.

4 COMMENTS:

  1. Well said R. Bwalya left footer magician japo watu awaoni mchango wake ila uyu mwamba is very talented

    ReplyDelete
  2. Kiungo bora kabisa kwa sasa anaye tumia guu la kushoto anaufanya mpira anavyo taka...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic