Uongozi
wa Simba uko kwenye mjadala wa kuamua timu yao iweke wapi kambi fupi kabla ya
kuanza msimu mpya wa 2014-15.
Afrika
Kusini na Oman ndiyo sehemu zinazotajwa kwa ajili ya kambi hiyo, lakini kuna
mambo mawili.
Oman kuna
joto kali sana ambalo wakati mwingine hufikia hadi nyuzi joto 40 na ushee,
hivyo Simba watalazimika kufanya mazoezi usiku tu joto linaposhuka.
Afrika
Kusini ni baridi kali kipindi hiki, wakati mwingine inakwenda hadi nyuzijoto 2.
Hivyo Simba watakuwa katika wakati mgumu na watalazimika kufanya mazoezi mchana
tu kwa kuwa asubuhi sana au usiku, joto ni kali sana.
Hivyo
Simba wako kwenye mjadala sehemu ya kwenda ingawa timu hiyo itaanza mazoezi
jijini Dar es Salaam kabla ya kufunga safari kwenda Zanzibar.
Baada
ya Zanzibar, Simba itaanza safari kati ya Afrika Kusini au Oman kutokana na
watakachokuwa wamefikia.







0 COMMENTS:
Post a Comment