West Ham imefanya kweli baada ya leo kumtangaza kiungo mkabaji wa
Barcelona, Alex Song ni mali yao.
Song amewasalimia mashabiki wa West Ham mara tu baada ya kutua London na
kusaini mkataba wa mkopo wa muda mrefu na klabu hiyo.
Mcameroon huyo mwenye umri wa miaka 26 alihaha kupata nafasi ya kudumu
katika kikosi cha kwanza cha Catalan.
Aliondoka Arsenal mwaka 2012 kwenda Camp Nou lakini ameamua kurejea tena
kwenye Barclays Premier na kujiunga na Wagonga nyundo hao wa London.
West Ham imeshinda vita ya kumpata baada ya klabu kadhaa kama Napoli ya
Italia na Galatasaray ya Uturuki nazo kuonyesha nia ya kumpata.
0 COMMENTS:
Post a Comment