Wadau mbalimbali wanaoipenda Barceloa, wamelaumu kupitia mtandao wa
kijamii wa Instagram kutokana na kitendo cha mshambuliaji Neymar kuonekana
akiwa juu ya ‘motabaiki’.
Neymar ametupia picha akiwa kwenye pikipiki, hali ambayo inaonyesha
kuwapa hofu mashabiki ambao wanaamini hajapona vizuri.
Baadhi wamemuunga mkono kwamba anastahili bata, lakini wengi
wakasisitiza anapaswa kuvuta subira.
Neymar alilazimika kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia baada ya
kuumizwa na beki wa Colombia na alikosa mechi za mwanzo za La Liga kutokana na
uti wake wa mgongo kuvunjika mfupa mdogo.
|
0 COMMENTS:
Post a Comment