Kocha na beki wa zamani wa Simba, Amri Said ‘Jaap Stam’ ambaye alikuwa msaidizi wa
Patrick Phiri wakati akiinoa Simba mwaka 2010, amemuomba Phiri kuhakikisha
anamrejesha Haruna Moshi ‘Boban’ baada ya kuona upungufu kikosini hapo.
Boban
kwa sasa hana timu tangu aachane na Coastal Union, kwa sababu zake binafsi,
hata hivyo msimu uliopita alikuwa kwenye kiwango cha hali ya juu.
Stam
ambaye amewahi kuifundisha Ndanda FC, amesema Phiri ni kocha mwenye uwezo wa
kuishi na watu watukutu, ambapo alimudu kuishi naye mwaka 2010.
“Phiri
anamjua Boban, wengi wamekuwa wakishindwa kuishi naye kutokana na utukutu wake,
lakini kumbuka enzi zetu nikiwa na Phiri tuliweza kukaa naye na kufanya kile
Wana-Simba walitamani.
“Pamoja
na kwamba nimeondoka Simba, lakini ukweli ni kwamba Phiri anahitaji kuwa na mtu
kama Boban, maana anamfahamu vema utukutu na kiwango chake,” alisema beki huyo
wa zamani wa Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment