August 22, 2014





Na Saleh Ally
BAADA ya kucheza Ligi Kuu Bara kwa dakika 270 tu, Yanga na Simba watakuwa katika wakati mgumu na wenye presha ya juu.


Presha hiyo itawaangukia makocha Marcio Maximo wa Yanga na Patrick Phiri wa Simba ambao wanajua presha kubwa ya mechi hiyo ya watani.

Maximo:
Maximo hakuwahi kuifundisha klabu yoyote, hivyo huenda akawa ana presha ya juu zaidi kwa kuwa baada ya mechi tatu tu, anakutana na Simba ambao inawezekana angependa kukutana nao kikosi chake kikiwa kimeimarika zaidi.

Taarifa ni kwamba alikataa kucheza mechi za kirafiki hadi hapo atakapokuwa amekitengeneza vizuri kikosi chake. Inawezekana atakuwa amefanya hivyo kupitia mechi kadhaa za kirafiki atakazocheza kabla.

Lakini bado presha itakuwa juu wakati anaingia katika mechi hiyo dhidi ya Simba ambayo safari hii imekuwa mwanzoni badala ya mwishoni au katikati kama ilivyozoeleka.

Wachezaji wapya kama Coutinho na Jaja, lakini wale wa zamani kama Haruna Niyonzima, Mrisho Ngassa, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite na wengine, watataka kuonyesha umuhimu wao.


Hakuna ubishi, ratiba hiyo ambayo ni nzuri kwa maana ya changamoto ili kuepusha mazoea, itakuwa imekaa vibaya kwa Maximo.

Huenda litakuwa jambo zuri kwake kushinda mechi zake zote tatu za mwanzo dhidi ya Mtibwa Sugar (ugenini) na mbili za nyumbani Taifa dhidi ya Prisons na JKT Ruvu ambao ni wagumu kweli.

Phiri:
Anaweza asiwe na presha kubwa, lakini mechi ya watani na hasa Simba na Yanga haizoeleki, hivyo bado itakuwa imekaa vibaya hata kwake.

Kama ilivyo kwa Yanga, hata Simba kwa wachezaji wapya kama Modo Kiongera, Pierre Kwizera, Abdi Banda lakini hata wa zamani kama Amissi Tambwe, Joseph Owino, Ramadhani Singano ‘Messi’, watakuwa na presha pia.

Huenda kukawa na nafuu kidogo kwake kwa kupitia mambo mawili. Moja ni uzoefu wake na mechi hiyo ya watani, haitakuwa ya kwanza au ya pili kwake na amewafunga Yanga zaidi ya mara tatu.

Lakini Yanga hii ni chini ya Maximo, hajawahi kukutana nayo na kutakuwa na tofauti tu. Pili ni timu atakazoanza nazo, Coastal, Polisi Moro na Stand United. Mechi zote tatu watakuwa nyumbani Uwanja wa Taifa, maana yake watazoea vizuri zaidi hadi wanakutana na Yanga.

Lakini Coastal labda iwe imebadilika, Polisi na Stand, wote ni wageni, Simba ikiwa makini ina nafasi ya kuwakaribisha vizuri kwa vipigo ingawa haitakuwa sawa kuwadharau hata kidogo. Mfano mzuri ni Mbeya City msimu uliopita.

Kati yao wote, nani anaweza kuifikia mechi hiyo akiwa amejipatia pointi tisa, yaani ameshinda mechi zote tatu za mwanzo?

Kama kila timu itakuwa imefanya hivyo, basi itakuwa ni mechi nzuri ya kila upande kutafuta pointi 12 ambazo ikiwa ni sare, kila mmoja atafikisha 10. Akipigwa mmoja atabaki na 9 na mwenzake atapanda hadi 12.

Hii ndiyo sehemu inayozidisha presha na inaonyesha kweli mechi hiyo iwapo upande mmoja utapoteza na kushindwa kutulia, basi utajivuruga ligi nzima.

Kabla Yanga itakutana na…
Mtibwa Sugar - Moro
Prisons - Dar
JKT Ruvu - Dar


Kabla Simba itakutana na …
Coastal Union - Dar
Polisi Moro - Dar
Stand United - Dar

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic