Msimu mpya unaanza mwezi ujao, tayari makocha
wameanza kujua vikosi vyao vya kwanza, kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ ametajwa
kuwa ndiye atakuwa chaguo la kwanza katika kikosi cha Yanga, ikiwa na maana
kwamba amewapiga bao Juma Kaseja na Ally Mustapha ‘Barthez’.
Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo, ametamka wazi kuwa kipa
huyo ndiye atakaye kuwa changuo la kwanza, kutokana na kuwa na uwezo hasa
ikizingatiwa ndiye chaguo la kwanza katika timu ya taifa,Taifa Stars.
Maximo ameliambia gazeti hili, kuwa hawezi kuzungumzia
uwezo wa mchezaji mmoja-mmoja lakini kwa upande wa kikosi chake bado Dida
atakuwa namba moja.
“Kwa sasa naweza kusema kipa namba moja ni Dida, kutokana na kuwa na
kiwango bora, ndiyo maana hata timu ya
taifa wamemuamini na wamekuwa wakimtumia mara kwa mara lakini klabu
itategemeana na uwezo ambao atakaounyesha,” alisema Maximo.
Alikwenda mbali na kusema kuwa tayari kwake
amewapanga ambapo Juma Kaseja ni chaguo la pili huku Barthez akiwa wa tatu,
japo amesema wote wanaelekeana viwango.
Ikumbukwe katika msimu uliopita katika mzunguko
wa pili Dida alidaka takribani michezo yote na Barthez aliweza kusugua benchi
mpaka msimu ulipomalizika.
0 COMMENTS:
Post a Comment