August 25, 2014



Real Madrid imekubali kumuachia Angelo Di Maria ambaye anatua Man United kw akitita cha pauni milioni 64.

Uhamisho wake utavunja rekodi na kuwa ghali zaidi England ukiupita ule wa pauni milioni 50 wakati Fernando Torred alipotua Chelsea akitokea Liverpool.
Di Maria raia wa Argentina, anatarajia kutua jijini Manchester leo kwa ajili ya vipimo na kumalizana na wenyeji wake.
Kocha Carlo Ancelotti wa Madrid amethibitisha kwamba mkali huyo alikwenda kuwaaga mazoezini kwamba anaondoka.
Man United imekuwa ikifanya juhudi kujiimarisha baada ya kusuasua kwa msimu mzima na pia kuanza vibaya msimu mpya kwa kipigo na sare dhidi ya Swansea na Sunderland.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic