August 31, 2014



Mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Amissi Tambwe ameanza kuonyesha makali baada ya kupiga bao mbili katika mechi ya jana usiku Simba ilipoiadhibu KMKM ya Zanzibar kwa mabao 5-0.
Tambwe raia wa Burundi alipiga bao mbili na kuiwezesha Simba kuongoza kwa mabao 4-0 hadi mapumziko kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.

Wengine waliofunga mabao ni wakongwe Amri Kiemba na Shaaban Kisiga ambaye alipiga bonge la bao baada ya kupokea pasi ya Tambwe.
Kipindi cha pili, Elius Maguri naye alipiga bao la tano huku memba wa kundi la Friends of Simba (Fos) wakishuhudia uwanjani hapo.
Simba ilionyesha soka safi na la kuvutia katika kipindi cha kwanza lakini ikaendelea kuwapa kazi KMKM katika kipindi cha pili huku ikitumia vijana zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic