August 31, 2014



Beki Donald Musoti amekubaliana na uongozi wa Simba kuhusiana na suala lao la kutaka kumuacha.
Simba imechukua uamuzi wa kumuacha Musoti raia wa Kenya na nafasi yake ichukuliwe na Mganda Emmanuel Okwi.
“Kila kitu kimekwenda vizuri na tayari Musoti ameambiwa naye amekubali kuhusiana na hilo.
“Kawaida linaweza lisiwe jambo zuri sana kwa mtu yoyote, lakini amekubali na hakuna ulalamishi wala nini,” kilieleza chanzo kutoka Simba.
Awali Musoti aliiambia Blog hii ya wanamichezo kwamba atasubiri iwapo watamueleza basi hatakuwa na kipingamizi kama kila kitu kama taratibu kitafuatwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic