Wanachama 860 wa Simba leo wamemfuta na kumfukuza aliyekuwa
mgombea wa Urais wa klabu hiyo Michael Richard Wambura.
Uamuzi huo umefikiwa leo kwenye mkutano wa wanachama wa Simba uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Wambura na wanachama wengine 72 wamefukuzwa kutokana na kukiuka na kupeleka masuala ya soka mahakamani.
Kabla ya kufikia uamuzi wa kufanya mkutano, Simba kupitia kwa
Rais wake, Evans Aveva ilitoa nafasi kwa wao kumuona na kuwasilisha utetezi
wao.
Hata hivyo, hakuna hata mwanachama mmoja aliyejitokeza kwa ajili
ya kulizungumzia suala hilo.
Uongozi wa Simba umesema, pamoja na kutojitokeza, wengine
walikuwa wakifanya kampeni kuzuia uchaguzi huo kufanyika, wakipanga tena kwenda
mahakamani.
Wanachama hao 72 walikwenda mahakamani kupinga Wambura
kuenguliwa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba chini ya Dokta Damas Daniel Ndumbaro.
0 COMMENTS:
Post a Comment