Taifa Stars imeondolewa
kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa mara nyingine tena.
Kwa mara ya pili mfululizo
inatolewa na Msumbiji baada ya kufungwa mabao 2-1.
Katika mechi hiyo mjini
Maputo, wenyeji walipata bao lao katika dakika ya 45 mfungaji akiwa Josemar.
Kipindi cha pili, Stars
walisawazisha katika dakika ya 77 kupitia Mbwana Samatta.
Baada ya hapo, mashambulizi
yalikuwa ya zamu na kila upande ukionyesha kupania kushinda.
Stars ndiyo walikuwa
wakihitaji ushindi zaidi wakati Msumbiji wangevuka hata kwa sare ya bao 1-1
baada ya ile sare ya mabao 2-2 jijini Dar es Salaam.
Elias Pelembe, mchezaji
ambaye amekuwa akiionea Taifa Stars, alifunga bao la pili katika dakika ya 84.
Pelembe maarufu kama
Domingues ndiye alimaliza kazi hiyo na sasa Stars imeng’olewa kwa jumla ya
mabao 4-3.
Mara ya mwisho, Stars iling’olewa
kwenye michuano hiyo mjini Maputo kwa changamoto za mikwaju ya penalti baada ya
sare ya mabao 1-1 Dar na Maputo.
0 COMMENTS:
Post a Comment