DK SUFIANI (KULIA) AKIPAMBANA NA SHABIKI HUYO ALIYETOA MANENO YA KEJELI... |
Daktari wa Yanga, Juma Sufiani, uvumilivu
ulimshinda hadi kufikia kutaka kuzichapa kavukavu na shabiki.
AKIMSHUGHULIKIA SHABIKI HUYO... |
Yanga ilifungwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa
Jamhuri na shabiki huyo alitupa maneno ya kejeli akidai ana uchungu wa Yanga
kufungwa.
Sufiani alijaribu kumsihi, lakini baadaye
alishindwa kujizuia na kuamua kupambana nae.
Hata hivyo, mmoja wa mashabiki maarufu wa
Yanga alijitokeza na kumzuia.
“Muache nimfunze adabu
kenge huyu, hanijui kama mimi ni mtoto wa mjini kuliko yeye, muache kwanza
nimpe vitasa vingine, hawezi kutuletea dharau zake za kilevi hapa, kwani nani
anayefurahia kufungwa hapa?” alisema Dk Sufiani akionyesha kuwa na hasira.
AKIAMULIWA... |
Sufiani alionyesha kukerwa na maneno ya shombo
ya shabiki huyo aliyekuwa na hasira ya Yanga kufungwa katika mechi ya ufunguzi
wa Ligi Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment