Mapenzi
kwa Chelsea yameshindikana kufichika kwa kiungo Frank Lampard, kwani alitaka
kumwaga chozi.
Lampard
amekiri kwamba alishindwa kujizuia na ilikuwa nusura amwage chozi baada ya
kuifungia Man City bao la kusawazisha dhidi ya Chelsea akiwa anatokea benchi.
“Kweli
nilijisikia vibaya lakini mimi ni mchezaji wa kulipwa, ninatakiwa kuonyesha
hilo.
“Ilikuwa
ni lazima niingie na mpira wa krosi niliopigwa na Milly ulikuwa bora, ulikuwa
ni lazima niutendee haki.
“Nimefurahia
kuifungia timu ninayoitumikia, lakini sijafurahia kuifanyia hicho Chelsea.
“Nimekuwa
pale kwa misimu 13 yenye mafanikio na mapenzi makubwa kwa mashabiki, lazima
nitajisikia vibaya,” alisema Lampard.
Chelsea
chini ya bosi Jose Mourinho ilimuuza Lampard Marekani na baadaye akarejea Man
City kwa mkopo.
Jana
alisawazisha na kufanya matokeo ya mwisho kati ya wenyeji Manchester City
waliokuwa pungufu baada ya Zabaleta kulambwa kadi nyekundu na Chelsea kuwa sare
ya 1-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment