MWESIGWA |
Ukishangaa ya usiyemjua, utayaona ya TFF.
Sasa imeibuka na jipya na kutaka Yanga, Simba na klabu nyingine 12 za Ligi Kuu
Bara, zikatwe 5% ya fedha za udhamini, ziingie TFF.
Uongozi wa TFF umeandika barua kwenye bodi
ya ligi ukitaka ulipwe 5% ya fedha za udhamini kutoka Vodacom na Azam TV ipewe
yenyewe.
TFF imetaka fedha hizo ili izitumie kwa
ajili ya maendeleo ya soka au timu ya taifa.
Lakini hali imezishitua baadhi ya klabu
ambazo zimeanza kuhoji chinichini kuhusiana na suala hilo.
Suala hilo la kushangaza kama litapita
litakuwa ni la aina yake kwa klabu kutoa fedha zao za udhamini na kulipa
shirikisho.
Suala hilo ambalo limeonekana litakuwa la
kwanza kufanyika katika ulimwengu wa soka, bado haijajulikana kama
limepitishwa.
Barua hiyo ya Septemba 19 kutoka TFF ikiwa imesainiwa na Katibu Mkuu, Mwesigwa Celestine, imeitaka bodi ya ligi kupeleka fedha hizo za klabu 14 za ligi kuu kwenye akaunti ya shirikisho hilo.
TFF imesema fedha hizo zitaenda kwenye akaunt ya Maendeleo ya Michezo Tanzania ambayo hushughulikia timu ya taifa.
(Kimantiki Vodacom na Azam TV hazidhamini timu ya taifa, inadhaminiwa na Kilimanjaro Beer.)
0 COMMENTS:
Post a Comment