Mshambuliaji Genilson Santana maarufu kama Jaja amecheza mechi
yake ya kwanza akiwa na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar na kufanikiwa
kufunga bao.
Jaja amefunga bao hilo 58 katika mechi ya kirafiki ya kimataifa
wakati Yanga ikiwavaa Thika United ya Kenya.
Hilo ni bao lake la pili baada ya kufunga la kwanza akiichezea Yanga mechi ya kwanza ya kirafiki 'official' kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.
Wakati timu zilikwenda mapumziko bila mabao, Yanga ilirejea na
kupata bao hilo baada ya Jaja raia wa Brazil kupokea pasi ya Simon Msuva,
akawahaa mabeki kabla ya kuukwamisha mpira wavuni kwa mguu wa kushoto.
Mashabiki wa Yanga walimshangilia kwa nguvu Jaja wakati anatoka
katika dakika ya 74, Said Bahanuzi akiingia kuchukua nafasi yake.
Mechi ilikuwa ngumu katika kipindi cha kwanza, Yanga ikianza
kushambulia na kuwabana Wakenga hao, lakini kuanzia dakika ya 39 waliamka na
kuwapa Yanga wakati mgumu.
Kipindi
cha pili, Yanga walikianza vizuri, wakishambulia zaidi, lakini bado Thika
United walikuwa imara.
1.
DEO MUNISI ‘DIDA’
2.
JUMA ABDUL
3.
OSCAR JOSHUA
4.
KELVIN YONDANI
5.
NADIR HAROUB ‘CANNAVARO’
6.
MBUYU TWITE
7.
SIMON MSUVA/Hussein Javu (Dk 73)
8.
HASSAN DILUNGA/Hamis Thabit (Dk 46)
9.
JAJA/Said Bahanuzi (Dk 74)
10.
HARUNA NIYONZOMA
11.
COUTINHO/Nizar Khalfan (Dk 68)
0 COMMENTS:
Post a Comment