NDANDA SIKU ALIVYOINGIA MKATABA NA NDANDA FC |
Baada ya Ndanda FC kupata nafasi ya kushiriki
Ligi Kuu Bara, mashabiki wa timu hiyo wamejipanga kuhakikisha timu yao inaibuka
na ushindi katika mechi zao mbili za mwanzo.
Ndanda inayodhaminiwa na Bin Slum Tyres Ltd inatarajiwa kufungua Dimba Septemba 20,
kwa kucheza na Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage na baadaye itasafiri
mpaka Morogoro kupambana na Mtibwa Sugar.
Mdau wa
timu hiyo na pia meneja wa Uwanja wa Nangwanda Sijaona, John Mapunda, alisema mashabiki
hao wamejipanga kikamilifu kuhakikisha timu yao inakusanya pointi sita za
mwanzo ambapo watacheza ugenini.
“Tayari mashabiki wameshaanza kupanga mipango
ya kuhakikisha Ndanda inapata pointi sita za mwanzo ambazo ni muhimu
ukizingatia itakuwa inacheza ugenini.
“Katika kuhakikisha wanapata pointi hizo,
wamedhamiria kusafiri na timu yao popote itakapokwenda ili wakatoe sapoti ya
nguvu,” alisema Mapunda.
0 COMMENTS:
Post a Comment