Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Mbrazil,
Genilson
Santos ‘Jaja’, ndiye atakayehusika na penalti zote za klabu hiyo
zitakazotokea katika mechi baada ya kumkosha kocha mkuu, Marcio Maximo kwa
uwezo wake wa kupiga mipira hiyo.
Katika mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika
katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola jijini Dar, Maximo aliwateua wapiga
penalti watatu, Said Bahanuzi, Simon Msuva na Jaja na kuwapa zoezi maalum la
kupiga penalti dhidi ya makipa, Juma Kaseja na Ally Mustapha ‘Barthez’.
Jaja ndiye aliyeibuka kinara wa matuta baada
ya kupiga penalti kumi na kufunga tisa huku moja ikigonga mtambaa wa panya.
Bahanuzi naye alionyesha umahiri baada ya kufunga nane kati ya kumi huku Kaseja
na Barthez kila mmoja akidaka tuta mojamoja. Msuva alifunga sita kati ya kumi
na kukosa nyingine ambazo zilipaa na kudakwa na makipa.
Maximo ambaye alikuwa pembeni akishuhudia
zoezi hilo, alionyesha kufurahia uwezo mkubwa wa Jaja katika upigaji wa penalty,
jambo linalodhihirisha kuwa katika mechi kama itatokea penalti basi chaguo la
Maximo kuipiga ni Jaja.
0 COMMENTS:
Post a Comment