Kiingilio
cha chini kwenye mechi ya Ngao ya Jamii kuashiria uzinduzi wa msimu mpya wa
Ligi kati ya Azam na Yanga itakayochezwa Jumapili (Septemba 14 mwaka huu)
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000.
Mechi
hiyo itaanza saa 10 kamili jioni, na kiingilio hicho cha sh. 5,000 ni kwa viti
vya rangi ya kijani na bluu vitakavyochukua jumla ya watazamaji 36,000 katika
uwanja huo wenye viti 57,558.
Viingilio
vingine katika mechi hiyo ambayo itatumia tiketi za elektroniki ni sh. 10,000
kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa viti vya VIP C na B wakati viti
vya VIP A kiingilio ni sh. 30,000.
0 COMMENTS:
Post a Comment