MUSOTI (KUSHOTO) AKIWA MAZOEZINI NA WACHEZAJI WENGINE WA SIMBA. |
Hali ya wasiwasi imetanda
ndani ya Simba baada ya beki waliyemnasa hivi karibuni, Shafii Hassan, ili
kuchukua mikoba ya Mkenya , Donald Musoti, imebainika kuwa usajili wake
umegonga mwamba katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Habari za kuaminika kutoka
ndani ya Simba zimedai kuwa jina la mchezaji huyo halikuwemo katika orodha ya
majina ya timu hiyo yaliyopitisha na TFF kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu
Bara.
Chanzo hicho kilifafanua
kuwa inawezekana sababu moja wapo ambayo ilisababisha usajili wa mchezaji huyo
kukwama inaweza kuwa ni tatizo la mtandao.
“Usajili wa Shafii umekwama
TFF, hivyo hatutakuwa na naye tena katika hatua ya kwanza ya ligi kuu labda
mzunguko wa pili.
“Tatizo kubwa la usajili
wake kutofanikiwa inawezakana ni kutokana na kuchelewa kupelekwa kwa jina lake
TFF ambapo tulilipeleka katika dakika za mwisho kabisa ambazo pengine ‘system’
(TMS), haikuweza kupata data zake kwa wakati husika kutokana na matatizo ya
mtandao,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Kutokana na hali hivi Simba
sasa itakuwa imebakiwa na mabeki wanne wa kati ambao ni Joseph Owino, Joram
Mgeveke, Miraji Adam, Isihaka Khatib.
Hata hivyo, Owino ndiye
beki pekee kati ya hao mwenye uzoefu wa kucheza mashindano mbalimbali kuliko
wachezaji hao ambao ni chipukizi na hawajakomaa kukabiliana na mikikimikiki ya
ligi kuu.
0 COMMENTS:
Post a Comment