Wakati Yanga ikicheza mchezo wake wa kwanza wa
kirafiki jijini Dar es Salaam leo dhidi ya Thika United, Kocha Mkuu wa Yanga,
Marcio Maximo, amewakabidhi viungo, Nizar Halfan na Andrey Coutinho jukumu la kupiga
faulo.
Maximo amekuwa akiwapa mazoezi ya ziada
wachezaji hao ya jinsi ya kupiga faulo wanapokuwa katika programu za mazoezi
kujiandaa na ‘mikikimikiki’ ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho.
Katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika jana
Jumanne kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Loyola jijini Dar, Yanga walianza kwa mazoezi mepesi ya kupasha misuli kabla
ya Maximo kugawanya wachezaji katika vikosi viwili vilivyoingia uwanjani
kucheza soka.
Mara baada ya programu hiyo kumalizika, kocha
huyo aliwatenga wachezaji wake ambapo Nizar, Niyonzima na Coutinho walipewa
jukumu la kupiga faulo kwa kuwekewa ukuta na ‘rundo’ la wachezaji ila bado kila
mmoja alifanikiwa kutikisa nyavu za Dida mara mbili kati ya tatu walizopiga.
Kitendo hicho kinaonyesha wazi kwamba tayari
Maximo amewapanga wachezaji maalum kujiandaa na majukumu hayo pindi
yatakapotokea katika michezo yao kuanzia huu wa kirafiki unaopigwa leo jijini
Dar.
Licha ya majukumu hayo, Coutinho na Nizar ndiyo wanaoonekana
kupewa ‘mzigo mzito’ kwani katika mazoezi ya timu hiyo walipewa jukumu lingine
la kupiga kona zote, ambapo zile za upande wa kushoto zilikuwa zikipigwa kwa
ustadi na Mbrazil, Andrey Coutinho, huku zinazotokea upande wa kulia zikipigwa
na Simon Msuva au Nizar Khalfan.
0 COMMENTS:
Post a Comment