| SIKU AZAM TV ILIPOSAINI MKATABA WA KUIDHAMINI LIGI KUU BARA |
Runinga ya Azam TV yenye asili yake
Tanzania, sasa imeingiza maombi ya kutaka kudhamini Ligi Kuu Rwanda.
Azam TV ni kati ya wadhamini wa Ligi Kuu
Bara na ndiyo kampuni ya kwanza ya matangazo kuidhamini ligi hiyo nchini.
Habari za uhakika kutoka nchini Rwanda
zimeelezwa kuwa Azam TV imekuwa kwenye ushindani mkubwa na Tele 10 inayomiliki
TV na redio.
“Kweli kumekuwa na ushindani mkubwa, awali
tulielezwa Tele 10 wameshinda lakini tulipofika kwenye mkutano wa waandishi
ikashindakana mkataba kusainiwa,” kilieleza chanzo kutoka Rwanda.
“Lakini baadaye tukapata taarifa kwamba
mambo yalikwama kwa kuwa Azam TV ya Tanzania imetoa fedha nyingi zaidi.”
Championi Jumatano lilifanya juhudi za
kuupata uongozi wa runinga hiyo na Mkurugenzi Mkuu wa Azam TV, Rhys Torrington
raia wa Uingereza akathibitisha hilo.
“Sasa ninachoweza kusema ni kwamba tunawania
kupata udhamini wa Ligi Kuu Rwanda.
“Tunafanya hivyo kama kampuni nyingine za
Rwanda zinavyotaka nafasi hiyo,” alisema huku akisisitiza hana ufafanuzi zaidi
kwa kuwa wanasubiri majibu.
Kama itafanikiwa kupata udhamini huo, Azam
TV itaweka rekodi kuwa kampuni ya kwanza ya Tanzania kudhamini ligi ya nje.







0 COMMENTS:
Post a Comment